1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yaikosowa sera ya biashara ya nje ya Ulaya

6 Desemba 2023

China imesema leo kuwa sera ya biashara ya nje ya Umoja wa Ulaya kuelekea Beijing haina maana.

https://p.dw.com/p/4ZpbG
Mdahalo wa China na UIaya.
Mdahalo wa China na UIaya.Picha: Yin Bogu/Xinhua/AP/picture alliance/dpa

Kauli hii imejiri katika mkesha wa mkutano wa kilele wa ngazi ya juu katika mji mkuu wa China, Beijing.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema ikiwa Umoja wa Ulaya utaweka vikwazo vikali kwa uuzaji wa bidhaa za teknolojia nchini China kwa upande mmoja, na unatumai kuongeza pakubwa usafirishaji bidhaa  kwenda China kwa upande mwingine, hiyo haina maana.

Soma zaidi: Rais wa Belarus aelekea China kwa ziara ya pili mwaka huu

Mkuu wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell na Charles Michel, rais wa Baraza la Ulaya, watakuwa Beijing kesho Alhamisi kwa mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na China.

Utakuwa mkutano wa kwanza wa kilele wa ana kwa ana kati ya wakuu wa Umoja wa Ulaya na Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu Li Qiang tangu mwaka wa 2019 na mojawapo ya mada kuu ni biashara.