China yaoongoza katika utoaji hukumu ya kifo duniani
11 Aprili 2017Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Amnesty International Marekani imeshuka kutoka orodha ya mataifa matano yanayoongoza katika utaoji hukumu ya kifo huku mwaka uliopita ikiwanyonga watu 20 ambayo ni idadi ya chini tangu mwaka 1991. Kwa jumla idadi ya watu waliopewa hukumu ya kifo duniani kote ilipungua kwa asilimia 37 huku vikiripotiwa visa 1,032 pekee. Naibu mkurugenzi wa program kuhusu maswala ya dunia katika shirika hilo la Amnesty International James Lynch amesema hukumu nyingi za kunyongwa zilitolewa mwaka jana ni kutoka China, Iran, Saudi Arabia, Iraq na Pakistan.
Misri ilichukua nafasi ya sita kwa kuongezeka mara mbili walionyongwa kutoka 22 mwaka 2015 hadi 44 mwaka uliopita. Utalawa wa Abdel Fattah al –Sisi umelaumiwa kutokana na ongezeko hilo.Baada ya kuibuka taarifa mpya kuwa yapo matifa ambayo awali yaliweka seri kesi zake za adhabu ya kifo,shirika la Amnesty International limeshinikisha kuwepo uwazi zaidi katika utaoji hukumu ya aiana hiyo. Mwaka huu shirika hilo la kutetea haki za bindamu lilizindua ripoti kuhusu hukumu ya vifo iliyotolewa kisiri nchini China. Hata hivyo China imeshirikia kuwa mfumo wake wa sheria umekuwa wazi zaidi,japo shirika la Amnesty International limepinga vikali hilo. Barani Afrika adhabu za kunyongwa ziliongezeka kutoka 443 mwaka 2015 hadi elfu 1,086 hasa kutokana na ongezeko za hukumu hizo nchini Nigeria. Hatari ya watu kunyongwa kutokana na uhalifu ambao hawajatekeleza bado ni tishio huku nusu ya walioondolewa hatiani duniani kote mwaka 2016 wakitokea Nigeria.
Mwandishi:Jane Nyingi/AFPE/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga