1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China:Marekani ilipeperusha maputo zaidi 10 katika anga letu

14 Februari 2023

China imesema leo kwamba zaidi ya maputo 10 yaliachiwa na Marekani tangu mwezi Mei mwaka 2022 kuingia katika anga yake na anga ya mataifa mengine.

https://p.dw.com/p/4NTRM
China I Wang Wenbin I Sprecher des chinesischen Außenministeriums
Picha: Kyodo/picture alliance

Waziri wa mambo ya kigeni wa China Wang Wenbin amesema maputo hayo yaliyorushwa katika maeneo mengi ya dunia na yakaingia katika anga yake mara kumi kinyume cha sheria. 

Wang hakutoa taarifa zaidi za mataifa mengine yalikoonekana maputo hayo.

Alikataa pia kutoa majina ya maeneo maputo hayo yalipoonekana nchini China au hata kutoa picha za kuthibitisha hilo. Tayari Marekani imekanusha tuhuma hizo.

Soma pia:China yaishtumu Marekani kutumia nguvu baada ya puto lake kudunguliwa

China na Marekani zimekuwa zikitupiana maneno tangu Marekani ilipodungua puto kubwa la China, katika eneo la bahari la Carolina baada ya kudaiwa kufanya ujasusi katika maeneo ya kijeshi ya Marekani.