1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Corona: Wanawake Tanzania walia athari za COVID19 kibiashara

Salma Mkalibala25 Juni 2020

Wanawake mkoani Mtwara nchini Tanzania wamesema wanaathiriwa na janga la virusi vya corona kiuchumi na kijamii na kueleza biashara zao kuyumba kimtaji, kushindwa kuendeleza biashara.

https://p.dw.com/p/3eL05
Tansania Dar es Salaam | Coronavirus | Beerdigung Gertrude Rwakatare, Politikerin
Picha: DW/S. Khamis

Wengine wanahofia taasisi za mikopo na mabenki yatachukua mali zao  na kuuziwa kutokana na kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati.

Hayo yameelezwa kwenye Kongamano maalumu la kujadili athari za janga la virusi vya corona kwa wanawake lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la kimwamu na kufadhiliwa na mfuko wa wanawake Tanzania, ambapo wanawake wanaojihusisha na shughuli mbalimbali wamekutanishwa.

Akianza kuelezea suala la kuyumba kwa kibiashara Kuruthum Thomas ambaye ni mpishi wa chakula amesema awali alikuwa na uwezo wa kupika chakula zaidi ya kilo kumi za wali wa pilau na aina nyingine lakini tangu janga la corona litokee amekuwa akipika kilo nne na kushindwa kumaliza.

Janga la corona limewaathiri vipi vijana Tanzania?

Janga la corona limeyaathiri vipi maisha ya vijana Tanzania?

Naye Batuli Kindimbo ambaye ni mmiliki wa saluni amedai biashara yake imeyumba na kupekelea kushindwa kurejesha kwa wakati fedha za mkopo ambazo alipata kwenye taasisi ya fedha huku akijawa na hofu kuwa huenda mali zake ambazo aliweka dhamana kwenye taasisi hiyo zikachukuliwa na kupigwa mnada.

Kwa kuwa wengi wameshindwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida kutokana na janga la corona, wapo wanaohofia watashindwa kulipa madeni na taasisi za mikopo huenda ikachukua mali zao.
Kwa kuwa wengi wameshindwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida kutokana na janga la corona, wapo wanaohofia watashindwa kulipa madeni na taasisi za mikopo huenda ikachukua mali zao.Picha: DW/S. Khamis

Wakizungumzia upande wa kijamii, Deogratius Makoti na Fidea Ruanda ambao ni wawezeshaji katika kongamano hilo wamesema janga la corona limeathiri shughuli za kijamii ngazi ya familia hadi serikalini kutokana na kusitishwa kwa huduma mbalimbali kama zoezi la usajili wa vitambulisho vya taifa kwa kuwa lilisimama kwa muda na kusababisha baadhi ya akina mama kushindwa kuendelea kufuatia haki zao kwenye masuala ya mirathi.

COVID-19 yasababisha changamoto tele

Salma Irigo ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kutoka katika dawati la jinsia na watoto wilaya ya Mtwara, ametaja changamoto kadhaa walizozibaini katika kipindi hiki cha cha ugonjwa wa covid 19.

Hata hivyo kwa upande wa idara ya ustawi wa jamii imesema imechukua tahadhari na kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na corona kwa watu wote huku ikisita kusema athari walizozishuhudia kutokana na janga hilo. Kama anavyoeleza Neema Silas ambaye ni ofisa ustawi.