DAVOS : Rais Lula ataka muafaka wa biashara duniani
26 Januari 2007Rais Inancio Lula da Silva wa Brazil leo hii ametowa wito wa kwa nchi tajiri duniani kutourudisha nyuma ulimwengu wa nchi zinazoendelea kwa kugoma kufikia maridhiano juu ya mkataba wa biashara dunaini wakati muda wa kufikia maafikiano ukiyoyoma.
Mawaziri wa biashara wa nchi 30 wamekusanyika kwenye Kongamano la Kiuchumi Duniani huko Davos katika juhudi za kufufuwa mazungumzo ya biashara duniani ya duru ya Doha kwa kupunguza ushuru wa bidhaa,ruzuku na vikwazo vyengine vya biashara.
Lula amesema ni muhimu zaidi kwa nchi za Uingereza, Ufarasa,Ujerumani ambazo zina dhima muhimu kuwajibika katika kufikia muafaka wa mazungumzzo ya biashara ya duru ya Doha ambayo amesema ni matumaini ya mamilioni ya watu wanaosubiri.
Lula ambaye anaongoza taifa kubwa kabisa la Marekani ya Kusini amesema Brazil iko tyarai kufikia maridhiano na amezitaka hususan Ulaya na Marekani kuchukuwa hatua kama hiyo.