Dortmund imeshinda mabao 3-0 dhidi ya Club Brugge
19 Septemba 2024Ni katika mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya. Dortmund, iliyopoteza mechi ya fainali ya michuano hiyo ya Ulaya msimu uliopita mbele ya miamba Real Madrid, ilifunga bao la kwanza kunako dakika ya 76 kabla ya Gittens kufunga bao lake la pili katika dakika ya 86 ya mchezo. Mshambuliaji mpya Serhou Guirassy aliyejiunga na Dortmund akitokea Stuttgart ambapo alifunga mabao 28 katika mechi 28 za ligi kuu ya Bundesliga msimu uliopita, alifanyiwa madhambi kwenye kisanduku cha 18 na kufunga penalti ya dakika za lala salama.Gittens amekiambia kituo cha habari za michezo cha DAZN kuwa, anajisikia vizuri baada ya kupata ushindi na kwamba aliingia uwanjani akiwa na nia ya kufanya mabadiliko kwenye mchezo. Nahodha wa Dortmund Emre Can amemwagia sifa raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20, akieleza kuwa alileta nguvu mpya na kusaidia kubadili mwelekeo wa mchezo.