1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Somalia na Ethiopia hayajafua dafu

14 Agosti 2024

Duru ya pili ya mazungumzo baina ya Somalia na Ethiopia chini ya upatanishi wa Uturuki imemalizika bila ya kufikiwa mapatano. Hata hivyo Uturuki na mawaziri wa nchi hizo za Afrika bado wanayo matumaini.

https://p.dw.com/p/4jS6k
Somalia |  Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somalia Hassan Sheikh MohamudPicha: REUTERS

Mgogoro kati ya Somalia na Ethiopia umesababishwa na hatua ya Ethiopia ya kukodi eneo la ufukweni la kilometa 20 la Somaliland.

Kwa upande wake Ethiopia inautambua uhuru wa Somaliland ambayo hapo awali ilikuwa sehemu ya Somalia.

Somalia na Ethiopia zafanya mazungumzo nchini Uturuki

Somalia imesema mkataba huo unaenda kinyume na sheria na imelipiza kisasi kwa kumtimua balozi wa Ethiopia, na pia imetishia kuwatimua maalfu ya wanajeshi wa Ethiopia waliopo nchini Somalia kusaidia kupambana na waasi.