1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congo: wahudumu wa afya wanufaika na ugonjwa wa Ebola

Saleh Mwanamilongo
6 Agosti 2021

Wahudumu wa afya walichangia ongezeko la machafuko wakati wa vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola, inaelezea ripoti ya shirika la utafiti kwa ajili ya Congo (GEC).

https://p.dw.com/p/3ydKu
Kongo Ebola Ausbruch
Picha: Reuters/O. Acland

Ripoti hiyo ya kurasa 35 inaelezea jinsi juhudi za kupambana na ugonjwa wa Ebola zilivurugwa na maafisa wanaohusika na usalama pamoja na huduma za afya. Shirika la Utafiti kwa ajili ya Congo la Chuo Kikuu cha NewYork, Marekani, linaelezea kwenye ripoti hiyo kuwa ugonjwa huo uliodumu miaka miwili ulitokana pia na kile inachoita kuwa ni Biashara ya Ebola.

Tresor Kibangula, mtafiti mkuu kwenye shirika la Congo Reseach Group amesema juhudi za kitaifa na  kimataifa katika kupambana na ugonjwa wa Ebola, ziliathirika sio tu na machafuko, zilichangia kuweko na mzozo zaidi huko Kivu ya Kaskazini.

''Ni raia waliyoita kuwa Ebola Business, kutokana na kwamba baada ya miaka mingi ya vita serikali au jamii ya kimataifa haijashughulikia vita hivyo, lakini ulipozuka ugonjwa wa Ebola mamilioni ya fedha zilitolewa. Kwa jumla dola biloni moja zilitolewa kwa ajili ya Ebola na hiyo ilichangia kuchochea zaidi machafuko.'' alisema Kibangula.

 Shirika la WHO lakanusha tuhuma

Zaidi ya watu elfu tatu waliambukizwa Ebola na wengine zaidi ya Elfu mbili kufariki  mnamo kipindi cha miaka miwili
Zaidi ya watu elfu 3 waliambukizwa Ebola na wengine zaidi ya Elfu 2 kufariki mnamo kipindi cha miaka miwiliPicha: picture-alliance/dpa/Bildfunk/AP/A.-H. K. Maliro

Ripoti hiyo ilionya pia kuhusu malipo yaliyotolewa na baadhi ya wahudumu wa afya kwa pande hasimu huko Beni. Ili kuyafikia maeneo yaliyodhibitiwa na wapiganaji, ripoti imeelezea kwamba maafisa wa kamati ya kupambana na ugonjwa wa Ebola walikuwa wakifanya mazungumzo na viongozi wa makundi ya wapiganaji. Lakini Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, limekanusha madai hayo ya shirika la GEC na kusema maafisa wake hawakuhusika na malipo kwa kundi lolote la wapiganaji au kushirikiana na maafisa wa Congo wa idara ya upelelezi.

Raia kupoteza imani kwa wanajeshi wa Monusco?

Ripoti hiyo imesema raia wengi huko Kivu hawana imanai na wanajeshi wa kulinda amani ywa Umoja wa Mataifa, Monusco. Tresor Kibangula amesema utafiti uliondeshwa na shirika la GEC umeonyesha kuwa asilimia kuwa ya raia wametegemea kuwa usalama wao unatokana hasa na Mwenyezi Mungu kuliko wanajeshi wa Monusco.

Kibangula aliendelea kusema :''Matokeo ya utafiti wa GEC huko Beni na Butembo umeonyesha kuwa wakaazi wa huko wanaimani hasa na wanajeshi na makundi ya wapiganaji kuliko wanajeshi wa Monusco. Hawaamini kwamba watu waliotoka mbali wanaweza kuwalinda.''

Mwaka 2018, jimbo la Kivu ya Kaskazini lilikumbwa na ugonjwa wa Ebola ulisababisha vifo vya watu 2,270 kwa kipindi cha miaka miwili.