1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fayulu: Polisi imetumia risasi kuwatawanya waandamanaji

27 Desemba 2023

Martin Fayulu mmoja ya wagombea wa urais katika uchaguzi wa Kongo, ameishutumu polisi nchini humo kutumia risasi za moto kuwatawanya watu mjini Kinshasa, walioshiriki maandamano yaliyoitishwa na upinzani.

https://p.dw.com/p/4ad8I
Kongo Kinshasa 2023 | Polisi ikitawanya mikusanyiko ya waandamanaji wanaounga mkono upinzani mjini Kinshasa.
Polisi ikitawanya mikusanyiko ya waandamanaji wanaounga mkono upinzani mjini KinshasaPicha: John Wessels/AFP/Getty Images

Maandamano hayo yaliyoitishwa na upinzani ya kutaka uchaguzi urudiwe upya, kufuatia madai kwamba uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu. 

Akishikilia risasi mkononi mwake, Fayulu aliliambia shirika la habari la The Associated Press kwambailianguka karibu nayealipokuwa ndani ya makao makuu ya chama chake mjini Kinshasa wakati wa makabiliano ya polisi na waandamanaji. Hata hivyo madai yake hayakuweza kuthibitishwa. 

Soma pia:Polisi yazuwia maandamano ya upinzani Kinshasa

Polisi kwa upande wake wamesema hakuna risasi zozote za moto zilizotumika isipokuwa gesi za kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji. 

Martin Fayulu ni miongoni mwa wagombea watano wa upinzani walioitisha maandamano ya leo. Makundi ya kutetea haki za binaadamu na waangalizi wa kimataifa wa uchaguziwanamashaka pia na uchaguzi uliofanyika na kusema hatua ya kurefushwa kwa shughuli ya uchaguzi huo haikuwa halali.