SiasaNigeria
Frank-Walter Steinmeier aendelea na ziara yake Afrika
13 Desemba 2024Matangazo
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anaendelea na ziara yake katika mataifa matatu ya Afrika. Baada ya Nigeria, Steinmeier ameelekea nchini Afrika Kusini na baadae Lesotho.
Rais huyo wa Ujerumani anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na kujadili kuhusu kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kimkakati baina ya nchi hizo mbili.
Akiwa Nigeria, Steinmeier alikutana na rais Bola Tinubu na kujadiliana kuhusu fursa za biashara ambapo Tinubu alisisitiza kuwa Nigeria imeanzisha mageuzi ya kodi na kupunguza urasimu, hatua iliyopongezwa na rais Steinmeier.