G7 inahitaji kusimama kudhibiti ukuaji wa China kiviwanda
22 Mei 2024Matangazo
Le Maire ameyasema hayo kabla ya kuanza mkutano wa kundi hilo nchini Italia siku ya Ijumaa na Jumamosi wiki hii.
Waziri huyo wa fedha wa Ufaransa amesema kundi la G7 pia linapaswa kuwa na msimamo wa pamoja juu ya mali za Urusi zinazozuiwa na kwamba Ufaransa iko tayari kufanyia kazi pendekezo la Marekani kutumia mali hizo kuipa mkopo Ukraine.
Wakati tofauti ya kiuchumi kati ya Ulaya na Marekani ikizidi kukuwa, Le Maire amesema pia Ulaya inahitaji kuondokana na hali ya kujikokota kiuchumi na kukuza mara dufu viwango vyake vya ukuaji katika miaka kadhaa ijayo.