JamiiGambia
Gambia yashikilia uamuzi wa kupiga marufuku ukeketaji
16 Julai 2024Matangazo
Shirika la afya duniani WHO na lile la kuwahudumia watoto UNICEF wametoa taarifa ya pamoja Jumatatu jioni wakiipongeza Gambia kwa hatua ya kuzuia muswada uliolenga kuondoa marufuku ya wanawake kukeketwa.
Mashirika hayo ya kimataifa yamesema hatua hiyo inathibitisha kwa mara nyingine ahadi za Gambia katika masuala ya haki za binadamu, usawa wa kijinsia, na kulinda afya na ustawi wa wasichana na wanawake.
Wabunge nchini Gambia walipiga kura ya kutupilia mbali muswada huo. Mwaka 2015, kiongozi wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh alipiga marufuku vitendo vya ukeketaji, lakini wanaharakati wanasema utekelezaji wa sheria hiyo umekuwa dhaifu na wanawake wanaendelea kufanyiwa vitendo hivyo.