Wabunge nchini Gambia waunga mkono ripoti dhidi ya ukeketaji
9 Julai 2024Kamati ya pamoja ya afya na jinsia iliwasilisha mrejesho wake Jumatatu ikisema marufuku ya mwaka 2015 dhidi ya ukeketaji wanawake inapaswa kudumishwa kuzuia tohara ya wanawake kwa aina zote nchini Gambia.
Ukeketaji unahatarisha maisha ya wanawake na wasichana
Ripoti hiyo imeendelea kusema kuondoa marufuku ya ukeketaji wanawake kunawaweka wanawake na wasichana katika hatari kubwa za kiafya pamoja na kukiuka haki yao ya ustawi wa kimwili na kiakili.
Soma pia:HRW yawataka wabunge wa Gambia kutoruhusu ukeketaji
Kamati hiyo imesema imeshauriana na wasomi wa Kiislamu waliothibitsha kuwa tamaduni hiyo sio hitaji la Uislamu, hoja ambayo hutumiwa sana na wanaharakati wa ukeketaji.
Ripoti dhidi ya ukeketaji wanawake yaidhinishwa kwa wingi wa kura
Baada ya mabishano makali ambayo wakati fulani yalizua kelele, wabunge 35 walipiga kura kuidhinisha ripoti hiyo, huku 17 wakipiga kura ya kuipinga na wawili wakikosa kupiga kura.