1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalaani viwango vya juu vya riba dhidi ya nchi maskini

4 Machi 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezitupia lawama nchi tajiri duniani na kampuni kubwa za nishati kwa kuyakandamiza mataifa maskini kwa viwango vya juu vya riba na bei ya juu ya mafuta

https://p.dw.com/p/4OFfA
Schweiz, Genf | António Guterres im UN-Menschenrechtsrat
Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Guterres ameyasema hayo kuelekea mkutano wa kilele unaotarajiwa kuanza kesho mjini Doha, Qatar, na utakaoyajumuisha mataifa zaidi ya 40 yanayogubikwa na hali inayozidi kuwa mbaya ya umaskini.

Soma pia:Mataifa ya G7 yatakiwa kuzisaidia nchi masikini 

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameendelea kuwa mataifa tajiri yanapaswa kutoa dola bilioni 500 kwa mwaka kuyasaidia mataifa hayo masikini yaliyotengwa na soko la kimataifa kufuatia viwango vya juu vya riba wakati ambapo kampuni za nishati zikipata faida kubwa.