Guterres:Tuwajibike ili kuwa na dunia salama
18 Januari 2023Kuelekea katika matumizi ya nishati safi ni miongoni mwa mada kuu zilizotawala Kongamano la Kiuchumi mjini Davos.
Akihutubia mkutano uliowaleta pamoja wanasiasa,wafanyabiashara na wataalamu wa masuala mbalimbali ikiwemo mazingira Guteres alionesha uwiano kati ya makampuni ya mafuta na yale ya tumbaku.
Makampuni hayo ambayo yamekubwa na kesi kadhaa kubwa za kisheria kuhusu athari mbaya zinazoshuhudiwa za hali yahewa ameyataja yamefanya "uongo mkubwa" juu ya mchango wao katika kuongezeka kwa joto.
Soma pia:Davos mjadala watawala ushirika wa China kimataifa
Katika hotuba yake ilioteka hisia za wengi alirejelea utafiti uliochapishwa na jarida la kisayansi la ExxonMobil ambalo lilitupilia mbali matokeo ya wanasayansi wake kuhusu nafasi ya nishati chafu katika mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea kuitesa dunia kwa sasa.
"Tunacheza na moto ya janga la hali ya hewa, kila wiki tunapata simulizi mpya za kutisha juu ya kuongezeka kwa utolewaji wa hewa chafu" Alisema mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa katika Kongamano la Davos.
Ameongeza kwamba ahadi za kukabiliana na ongezeko la joto karibu zitaangukia patupu ambapo bila jitihada zaidi kiwango cha ongezeko duniani kitashuhudiwa zaidi.
Akirejea juu ya mataifa yenye uchumi mkubwa katika kukabiliana na hali ya mazingira inayoshuhudia kiwango cha joto amesema dunia ipo kwenye hatari ya kutumbukia katika mgawanyiko mkubwa.
"Iwapo nchi zenye uchumi pale mataifa makubwa duniani kiuchumi yatakapotengana, hali itakayosababisha ofofauti wa kisheria,keknolojia,biashara na hata sarafu mbili zenye nguvu" Alisema Guterresh.
"Haya ni mambo ambayo hatutaki yatokee" Alisisitiza katika hotuba yake ambayo ilichota hisia za wengi katika kongamano hilo la uchumi la Davosi 2023.
EU:Tutahamasisha utolewaji wa ruzuku
Umoja wa Ulaya umesema utaendelea kuzihamasisha serikali katika umoja huo kutoa ruzuku kwa wafanyabiashara ili kupunguza idadi ya biashara zinazohamia Marekani, ikiwa ni mpango wake wa kuelekea katika nishati safi.
Katika kuangazia mchango waukuaji wa uchumi wa dunia kwa upande wa bara la Afrikalimeonekana kuwa na malighafi ya kutosha changamoto inayosalia ni usafirishwaji nje kwa uzalishaji.
Soma pia:Mamia waandamana Davos kupinga uroho wa mataifa tajiri
Wataalamu wamependekeza ushirika kati ya serikali na i na wawekezaji kushirikiana ili uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ufanyike ndani ya bara hilo.
Hotuba muhimu zinazosubiriwa
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky,wanatarahji kuhutubia kongamano hilo la uchumi la mwaka huu la Davos.
Hizi ni miongoni mwa hotuba muhimu katika jukwaa hilo kwa mwaka huu wa 2023 huku Ujerumani ikikabiliwa na shinikizo la kuipatia Ukraine vifaru vya kivita.
Soma pia:Vita vya Ukraine, mdororo wa uchumi kugubika kongamano la Davos
Ukraine imekuiwa ikipambana na vikosi vya Urusikatika maeneo ya kimkakati wakati vita hivyo vikielekea mwaka pili tangu ilipovamiwa na Urusi.
Soma pia:Scholz, Zelenskiy kulihutubia kongamano la uchumi la Davos
Scholz ni kiongozi pekee kutoka mataifa yalioendelea kiviwanda ya kundi la G7 kuhutubia kongamano hilo la kiuchumi kwa mwaka huu anawasili mjini Davos akiwa nawaziri mpya wa masuala ya ulinzi akijiandaa kuanza kazi kazi.