Guterres:wahisani endeleni kuchangia misaada ya kiutu
5 Mei 2022Aliyasema hayo nchini Nigeria, kituo cha mwisho cha ziara yake Afrika iliyomfikisha katika nchi tatu za Afrika Magharibi.
Guterres aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Abuja amesema nchi na mashirika ya wafadhili wanapaswa kuongeza msaada wao badala ya kuupunguza, ili kuepusha mkwamo katika shughuli za kiuchumia Afrika na kwingineko duniani.
Wakati uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ukiendelea, mataifa mengi yameelekeza msaada wao kwa Ukraine, ambayo kiongozi wake Volodymyr Zelenskiy amesema dola bilioni 7 zinahitajika kila mwezi kughariamia huduma za kiutu.
Soma Pia:Guterres aisifu Nigeria kwa kuwasaidia wapiganaji wa zamani
Guterres alisema hatua sahihi ni kuongeza kiwango cha msaada, sio kubadilisha unakoelekezwa kwa kufanya hivyo ni kuhujumu ushirikiano wa maendeleo katika maeneo mengine duniani.
Ziara ya Guterres Nigeria
Kabla ya kwenda Nigeria, Katibu Mkuu Antonio Guterres alizizuru nchi nyingine mbili za Afrika Magharibi, Senegal na Niger.
Nchini Nigeria kiongozi huyo alilitembelea eneo lakaskazini, ambako kundi la Boko Haram lenye itikadi kaliya Kiislamu limekuwa likiendesha uasi kwa miaka 12 sasa.
Madhila kwa wakaazi wa sehemu hiyo yamekithiri kutokana na mripuko wa ugonjwa wa Uviko-19, na takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu wasiopungua milioni 8.4 wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Lakini, kulingana na Priscilla Bayo Nicholas, mtaalamu wa masuala ya lishe anayefanya kazi na shirika moja la Umoja wa Mataifa, alisema kuna dalili kwamba mzozo wa Ukraine umeathiri kiwango cha fedha zinazotolewa kwa ajili ya misaada ya kiutu katika eneo hilo.
Akizungumza upungufu huo wa fedha za msaada, Katibu Mkuu Guterres alisema njia bora ya kushughulikia changamoto hiyo ni kufanya mabadiliko katika mfumo wa kifedha ulimwenguni, ambao alisema umeundwa na matajiri, kwa maslahi ya matajiri.
Soma pia:Guterres: Niger isaidiwe kukabiliana na makundi ya jihadi
Akiwa huko huko kaskazini mwa Nigeria Guterres alikutana na watu ambao siku za nyuma walikuwa wanamgambo wa kundi la Boko Haram, ambao sasa wamebadilika na kulipa kisogo kundi hilo, linaloshutumiwa kusababisha vifo vya watu 35,000na kuwafanya wengine takribani milioni 2.1 kuyakimbia makaazi yao.
Guterres alielezea mshikamano wa Umoja wa Mataifa na wahanga wa uhalifu wa kundi hilo.