1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier kusisitiza 'amani na haki' nchini Ukraine.

24 Desemba 2022

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kwenye hotuba yake ya Krismasi atatoa wito wa amani nchini Ukraine baada ya nchi hiyo kukumbwa na vita vilivyoingia katika mwezi wake wa kumi.

https://p.dw.com/p/4LOnY
ACHTUNG Sperrfrist 24.12.2022  00 Uhr / Steinmeier Weihnachtsansprache 2022
Picha: Tobias Schwarz/AP Photo/picture alliance

Katika hotuba kwa taifa ambayo itatangazwa siku ya Krismasi, ambayo ni Jumapili tarehe 25, Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anatarajiwa kutaja masikitiko yake kutokana na  ukosefu wa amani nchini Ukraine, miezi 10 tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake dhidi ya nchi hiyo.

"Matarajio yetu ya dhati ni kwamba amani itawale tena," mwisho wa kumnukuu.

Rais Steinmeier anatarajiwa kusema katika hotuba yake ya Krismasi kwa taifa, kulingana na nakala iliyoonekana na DW siku ya Jumamosi.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier
Rais wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: Tobias Schwarz/AP Photo/picture alliance

Katika matamshi hayo, rais wa Ujerumani atabainisha jinsi vita vya kikatili vya Urusi, vilivyoanza Februari 24, ambavyo vimesababisha mateso mabaya kwa watu wa Ukraine pamoja na hofu kwamba uhasama huo utaenea.

Hotuba kamili ya rais wa Ujerumani itaonyeshwa kwenye televisheni ya Ujerumani mwendo wa saa moja usiku, siku ya Jumapili.

Mwaka 2022 ni mwaka mgumu kiuchumi

Katika nakala hiyo ya hotuba, Steinmeier anakubali kwamba vita vya Ukraine pia vimeleta athari nyumbani, haswa kiuchumi. Lakini anabainisha jinsi serikali ilivyopunguza mizigo mizito kwa watu wake kulingana na mpango wa ruzuku ulioanzishwa ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za nishati.

Amesistiza kwamba Krismasi ni wakati mwafaka wa kuangalia mambo ambayo yanatupa matumaini.

Maswala ya hali ya hewa yanawahitaji vijana na wazee

Kuhusu maswala ya dharura ya hali ya hewa, Steinmeier anabainisha ni muhimu kwamba Wajerumani wabaki kwenye mkondo wa mpito wa nishati mbadala.

Mgogoro wa nishati, uliochochewa na vita, umesababisha kuanzishwa upanuzi wa muda wa vinu vitatu vya nyuklia na vinu kadhaa vya makaa ya mawe, ambavyo Ujerumani ilitarajia kuwa imevifunga kabisa hadi kufikia sasa.

Rais Steinmeier amesema licha ya kwamba yapo matatizo mengine kwa wakati huu lakini mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa hayajtpoteza udharura wake pia. Hayawezi kusubiri na yanatuhitaji sisi sote kuyashughulikia.

Ujumbe wa matumaini

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier atamalizia hotuba yake kwa kubainisha jinsi wananchi walivyofanikiwa, licha ya vikwazo katika mwaka huu kuliko ambavyo wengi wangefikiria.

"Tulitenda kwa dhamira wakati msaada wetu ulipohitajika. Tulisaidiana. Ninajivunia nchi yetu.

Kilicho katika msingi wetu, kile ambacho kimetufanya kuwa na nguvu siku zote, kitaendelea kuwepo: sisi ni wabunifu, wenye bidii na tayari kuendeleza mshikamano. Tunaweza kupata nguvu na matumaini kutokana na haya katika mwaka mpya." mwisho wa kumnukuu.

Chanzo:DW