Hussein Mwinyi na Maalim Seif wakutana na rais Magufuli
14 Januari 2021Akizungumza wa wageni wake kutoka Zanzibar mbele ya waakazi wa Chato, Rais John Pombe Magufuli ameahidi kuwaunga mkono katika harakati zao za kuijenga Zanzibar mpya yenye umoja na mshikamano na uchumi imara na isiyokuwa na ubaguzi.
Katika ziara hiyo ambayo imeoneshwa na kurushwa moja kwa moja ya televisheni ya Taifa ya TBC viongozi hao walionekana kuwa na furaha katika kikao chao ambapo alipopewa nafasi ya kuzungumza Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi aliahidi kufanya kazi ya kwaunganisha wazanzibari.
Kwa upande wake Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamada mbali na kushukuru kupewa fursa hiyo alishukuru kuwa rais wa Jamhuri kuhubiri upendo na mshikamano na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za kuwaunganisha wazanzibari.
Hii ikiwa ni Mara ya kwanza kwa viongozi hao kukutana tangu kumalizika uchaguzi mkuu uliofanyika October mwaka jana, Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na umoja wa zanzibar chini ya serikali ya kitaifa huku akimuomba Maalim Seif kutumia uzoefu wake katika siasa kutoa ushirikiano wa dhati kwa Dk Mwinyi ili kuipaisha Zanzibar kiuchumi.
Mwandishi: Salma Said, Zanzibar