IAEA: Iran haiko wazi katika mpango wake wa nyuklia
14 Februari 2024Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za nyuklia, IAEA Rafael Grossi amesema Iran imejitenga na uwazi kuhusu mpango wake wa nyuklia, na hasa baada ya afisa wake aliyeongoza progamu ya nishati hiyo wa Iran, Ali Akbar Salehi hivi karibuni kutangaza ina uwezo wote wa uundaji wa silaha katika mamlaka yao. Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa viongozi wa serikali huko Dubai kiongozi huyo amesema hali hiyo inaongozea mkusanyiko wa mambo magumu katika eneo pana la Mashariki ya Kati wakati huu wa vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza. Baada ya kuvunjika kwa mkataba wa nyuklia wa 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani, inadaiwa kuanza urutubishaji wa nyuklia chini ya viwango vya kiwango cha uundwaji wa silaha.Lakini pia imekusanya uranium iliyorutubishwa vya kutosha kuunda silaha ikiwa inataka kufanya hivyo.