1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC inaashiria kupata nafasi ya kuwakabili watuhumiwa wa vurugu za uchaguzi nchini Kenya

Nina Markgraf31 Julai 2009

Serikali ya Kenya iliyogawanyika imeacha wazi uwezekano wa watuhumiwa wa uchaguzi wa 2007 kushitakiwa katika mahakama ya ndani ama nje ya nchi.

https://p.dw.com/p/J0mx
Waandamanaji wakati wa vurugu za uchaguzi Jan. 2, 2008 katika eneo la Mathare mjini Nairobi, Kenya.Picha: AP

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu-ICC iliyoko The Hague Uholanzi ipo tayari kutekeleza jukumu hilo endapo Serikali ya Muungano ya Kenya itashindwa kufanikisha jukumu hilo.

Wanaolengwa katika mjadala huu ni wale wote kwa namna moja ama nyingine walihusika katika vurugu baada ya uchaguzi ambazo zilisababisha watu 1,300 kupoteza maisha na wengine 300,000 kuyakimbia makazi yao.

Baada mjadala wa kutwa nzima wa serikali ya nchi hiyo kuhusu sakata hilo,imeelezwa mambo matano yamejadiliwa ingawa suala la kuunda mahakama maalumu lilikuwa jambo zito.

Baadae Rais Kibaki alisema itawafikisha mahakamni wale wote waliyochoche vurugu hizo zilizosababisha vifo vya watu.

Katika taarifa yake hiyo kwa umma Rais huyo ameahidi kufanya maboresho kwa vyombo vya dola vikiwemo mahakama,polisi na taasisi za uchunguzi ili kufanikisha haki kwa watuhumu na watuhumiwa.

Wachambuzi wanasema kushindikana kuundwa kwa mahakama hiyo kutasababisha matakwa ya ICC kuingila suala hilo kuashiria kupata nafasi.

Wanasema uwezo mdogo ulioneshwa na Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga katika kufikia umauzi wa kina katika suala hilo umepoteza mwelekeo wa Baraza zima la Mawaziri.

Ben Rawlence ambae ni Mtafiti kutoka shirika la haki za Binadamu la Kimataifa la Human Rights Watch amesema namna serikali inavyoendesha suala hili ni kuwaweka wakenya katika giza.

Amesema dhana ya Serikali ya nchi hiyo katika kufanikisha upatikanaji haki kwa kutumia mahakama ya ndani si jambo ambalo Wananchi walilitegemea.

Imefahamika kuwa kutokana na vurugu hizo zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka uliyopita watu mashuhuri nchini Kenya ikijumuisha baadhi ya Mawaziri wataweza kufikishwa kizimbani.

Kibaki na Kiongozi wa Zamani wa Upinzani nchini humo Raila Odinga walitofautiana katika uchaguzi wa Desemba 27 ambao Kibaki alijitangaza mshindi.

Baada ya vurugu zilizodumu kwa miezi kadhaa na kudhoofisha uchumi wa nchi hiyo hatimae waliunda serikali ya muungano ambapo hata hivyo mambo yameendelea kuwa tafarani.

Katika suala la utekelezaji wa haki kwa waliyohusika na vurugu hizo Kibaki na Odinga wanataka mahakama ya ndani wakati Wakenya wengi wanataka ICC wakiamini mahakama ya ndani haitotenda haki.


Mwandishi-Sudi Mnette RTRE

Mhariri.M. Abdul-Rahman.