1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

ICC yaongeza juhudi za kufufua kesi dhidi ya Joseph Kony

24 Novemba 2023

Majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC wamepiga jeki juhudi za waendesha mashitaka waliomba kusikilizwa kwa mashtaka wanayolenga kuyawasilisha dhidi ya mbabe wa kivita wa Uganda aliye mafichoni Joseph Kony.

https://p.dw.com/p/4ZQNE
Kiongozi wa kundi la LRA Joseph Kony kushoto akiwa na makamu wake Vincent Otti
Kiongozi wa kundi la LRA Joseph Kony kushoto akiwa na makamu wake Vincent OttiPicha: Stuart Price/dpa/picture alliance

Kupitia uamuzi wa mpito ulitolewa na mahakama hiyo yenye makao yake mjini The Hague, majaji wameridhia waendesha mashtaka wawasilishe hati yenye makosa yanayomkabili Kony bila mtuhumiwa huyo kuwepo mahakamani.

Hata hivyo majaji watalazimika kutafuta njia za kumfahamisha Kony kuhusu mashtaka hayo kabla ya kuamua kuisikiliza kesi yake bila ya mbabe huyo wa kivita kuwepo mbele ya mahakama.

Soma pia:ICC kutoa uamuzi rufaa ya mbabe wa kivita wa kundi la LRA

Joseph Kony, mwanzilishi na kiongozi wa kundi la Lord's Resistance Army (LRA) ambaye alipambana na utawala wa Rais Yoweri Museveni kwa karibu miaka 20, ndiye mtuhumiwa anayesakwa kwa muda mrefu zaidi na ICC.

Waranti wa kukamatwa kwake ulitolewa mnamo mwaka 2005 kwa jumla ya makosa 33 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Wahanga wa maovu ya LRA wazungumzia masaibu yao