JangaUfaransa
Idadi ya vifo kufuatia kimbunga Chido Mayotte yafika watu 39
25 Desemba 2024Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa siku kumi baada ya visiwa hivyo kukumbwa na kimbunga hicho. Hata hivyo mamlaka husika imesema huenda maalfu wamepoteza maisha kutokana na madhara yaliyosababishwa na dhoruba hiyo.
Mamlaka imeeleza kuwa shughuli ya kuhesabu watu waliokufa inatatizika kutokana na baadhi ya familia kuwazika ndugu zao haraka. Kasi ndogo ya kupeleka misaada visiwani humo imewakasirisha wenyeji wa Mayotte, eneo maskini lililopo chini ya himaya ya Ufaransa.
Wakati huo huo Msumbiji, imeripoti vifo vya watu 94 vilivyotokana na kimbunga Chido wakati nchi jirani ya Malawi ikiripoti vifo 13.