Idadi ya vijana wanaonaswa kwa ugaidi yaongezeka Ulaya
11 Septemba 2024Kijana raia wa Austria aliyeuawa kwa kupigwa risasi wiki iliyopita baada ya kumfyatulia risasi polisi wa Ujerumani mjini Munich, anadhaniwa kuwa alishinikizwa na itikadi kali. Lakini Emrah I mwenye umri wa miaka 18, kutoka mji mdogo katika eneo la Salzburg, hana mazowea ya kuhudhuria ibada katika msikiti wa eneo lake, wala hakufuga ndevu au kuvaa magauni marefu.
Soma: Marekani inahofu kwamba kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS huenda linajiunda upya
Kidokezo pekee ambacho huenda kilielezea tabia yake mjini Munich ilikuwa mapema mwaka wa 2023, wakati polisi wa Austria, waliokuwa wakichunguza malalamiko kuhusu mapigano katika shule yake, walipopata video ya mchezo wa kompyuta kwenye simu yake. Katika video hiyo, alikuwa amepamba sehemu ya matukio na bendera ya kundi la wanamgamabo la Al Qaeda.
Lakini baada ya kutopata chochote kingine, polisi sasa inaamini kuwa katika kipindi cha miezi kadhaa, kijana huyo alishawishiwa kuwa na itikadi kali kupitia mtandao.Watu 6 wajeruhiwa katika shambulio jipya la kisu Ujerumani
Emrah I hayuko peke yake. Kati ya Machi mwaka 2023 na Machi 2024, watafiti katika Taasisi ya Washington ya Sera ya Mashariki ya Karibu, nchi zinazozunguka mwambao wa mashariki wa Bahari ya Mediterania, walihesabu visa 470 vya kisheria vinavyohusiana na kundi la IS. Vijana au watoto wadogo walihusika katika takribani visa 30 kati ya hivyo huku ripoti zikiongeza kuwa idadi hii inaweza kuwa kubwa zaidi kutokana na kwamba mataifa mengi hayatoi takwimu ya umri wa waliokamatwa.
Ingawa kundi la IS lilishindwa kijeshi kufikia mwaka 2017, bado lipo. Uwepo wake ni pamoja na kuzuka upya kwa ukatili mkubwa na unaotisha katika mataifa ya Afrika na tawi lililoko Afghanistan linalojulikana kama Islamic State katika jimbo la Khorasan ambalo mara nyingi hujulikana kamaIS-K au ISIS-K. Waangalizi wanasema kwamba ISIS-K imekuwa ikilenga zaidi mawasiliano ya nje.
Tangu Januari mwaka huu, IS-K imewahimiza wafuasi wake kufanya mashambulizi ya mtu binafsi barani Ulaya na kulenga matukio makubwa kama vile michezo ya Olimpiki, matamasha na mechi za soka.
Lakini wataalam wanadhani ujumbe huo haujakusudiwa kwa vijana wa Ulaya peke yake. Wanaamini kuwa idadi inayoongezeka ya uvamizi unaofanywa na vijana unahusiana zaidi na jinsi mitandao ya kijamii na ile ya kutuma ujumbe inavyowawezesha vijana kufikia maudhui ya IS. Wanamgambo 15 wa kundi la IS wauwawa Iraq
Pieter Van Ostaeyen, mchambuzi ambaye amekuwa akifanya utafiti wa kundi la IS kwa zaidi ya muongo mmoja na ambaye pia analifuatilia kwa ajili ya shirika la utafiti la kimataifa la Mpango wa Kukabiliana na Itikadi Kali, anasema bado kuna kamandi kuu ambayo iliongoza kwa mfano, mashambulizi nchini Urusi. Ostaeyen ameongeza kuwa kwa sasa anadhani kuna mitandao tofauti zaidi ya kuwasajili vijana hao.
Moustafa Ayad, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mazungumzo ya Kimkakati ya Afrika, Mashariki ya Kati na Asia yenye makao yake mjini London ambayo inachunguza itikadi kali za kila aina, amethibitisha hilo na kusema ni zaidi ya mtandao mpana ambapo kuna watoto katika makundi yao ya mtandaoni, kwenye jamii hizo, wanaotaka kuwa washawishi.
Katika tukio la uwezekano wa shambulio kwenye tamasha za Taylor Swift huko Vienna, polisi wa Austria walichunguza mitandao ya kidijitali ya mshukiwa wa Austria mwenye umri wa miaka 19. Polisi wa Ujerumani kisha walimkamata kijana mwenye umri wa miaka 15 huko Brandenburg ambaye alishukiwa kumpa motisha kijana huyo wa Austria.Macron: Shambulio dhidi ya Sinagogi ni ugaidi
Ujumbe wa kimsingi ambao kundi la IS umekuwa ukishinikiza bado ni uleule: ''Ulimwengu unatesa Waislamu, lakini ukijiunga nasi, tutakuwa na nguvu pamoja.''
Wanasaikolojia wanasema kuwa vijana waliotengwa wanaotafuta mahala pa kujihusisha nako, huenda wakavutiwa na ujumbe wa aina hiyo.