Idadi ya waliojeruhiwa kwenye mkasa wa Magdeburg yaongezaka
23 Desemba 2024Matangazo
Katika mkasa huo watu watano waliuawa, akiwemo mvulana wa miaka tisa na wanawake wanne wakati mwanamume mmoja wa Saudi Arabia aliyetambuliwa kwa jina la Taleb A alipoendesha gari katikati ya umati wa watu katika soko la Krismasi siku ya Ijumaa jioni. Kufuatia mkasa huo ulioibua hisia kubwa,Chamacha mrengo mkali wa kulia cha AFD kinapanga kufanya maandamano na maombolezo katika mji wa Domplatz uliopo mashariki mwa Ujerumani. Mgombea wa ukansela wa chama hicho katika uchaguzi wa mwezi Februari Alice Weidel na wanasiasa kadhaa wa chama hicho katika ngazi ya jimbo watahudhuria. Tukio hilo limeibua pia masuala ya kisiasa. Andreas Bohs ni moja ya waliojitokeza kwenye maombolezo na haya ni maoni yake.