Kimbunga Gaemi chasababisha vifo vya watu 33 Ufilipino
26 Julai 2024Waliokufa Ufilipino ni pamoja na watu 11 walioangamia kwa kuzama maji au kupigwa shoti za nyaya za umeme katika mji Mkuu wa Manila uliokumbwa na moja ya mafuriko mabaya kuwahi kutokea zaidi ya muongo mmoja uliopita. Katika maeneo mengine maji yalijaa na kufinika nyumba hali iliyowasababishia baadhi ya wakazi kutafuta maeneo salama ya kukimbilia.
Barabara kuu zilikuwa hazipitiki na watu nusu milioni walikosa umeme mjini humo. Kulingana na Polisi watu 10 walikufa katika mikoa minne Kaskazini mwa mji wa Manila akiwemo mfanyakazi wa lori moja la mafuta lililozama katika mkoa wa Bataan baada ya kusombwa na mawimbi makubwa ya maji.
Kimbunga Doksuri chawahamisha maelfu China
Kuzama kwa lori hilo la mafuta kumesababisha mafuta kumwagika kote katika maji ya mafuriko na walinzi wa pwani wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana kudhibiti mgogoro wa kimazingira kufuatia janga hilo.
Kimbunga Gaemi kimesababisha mvua ya masika ambayo imekuwa ikishuhudiwa nchini Ufilipino tangu mwanzoni mwa mwezi Julai na kusababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi katika mikoa ya Kusini Mashariki mwa taifa hilo. Tangu mwezi huo zaidi ya watu milioni 1.3 wameathirika na hali hiyo mbaya ya hewa huku watu zaidi ya 211,000 wakipoteza makaazi yao.
Kimbunga Hagupit chaleta madhara Ufilipino
Kwa sasa kundi la waokoaji wanajaribu kuwatafuta wafanyakazi sita wa Meli iliyo na bendera ya Tanzania ya Fu-Shun, iliyozama katika eneo la pwani la Kaohsiung.