1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

IMF yaikopesha Pakistan ilipe madeni

13 Julai 2023

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeidhinisha mkopo wa dola bilioni 3 kwa Pakistan ili kuiwezesha nchi hiyo kuepuka kushindwa kulipa madeni yake.

https://p.dw.com/p/4TorW
Pakistan I Finanzen - IWF
Picha: Arif Ali/AFP

Pakistan inakabiliwa na mfumuko wa bei wa hali ya juu na bado inakabiliana na athari zilizosababishwa na mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo hivi karibuni.

Hata hivyo, kwa ajili ya kupewa mkopo huo IMF inaitaka Pakistan ifanye mageuzi ya kimsingi na iongeze juhudi za kukusanya kodi.

Soma zaidi: Imran Khan: Nchi maskini zitaathirika zaidi na Corona

Pakistan inakabiliwa na mgogoro mkubwa katika urari wa malipo na pia uhaba wa fedha za kigeni.

Mkopo huo wa IMF utatolewa kwa muda wa miezi tisa.