UchumiIndia
India yaiomba Marekani kuachia fedha zake dola milioni 26
31 Agosti 2023Matangazo
Kwa mujibu wa duru za serikali ya India, Marekani ilizizuia fedha hizo kutokana na makampuni hayo kudaiwa kufanya biashara na Kampuni kubwa ya almasi ya Urusi iliyowekewa vikwazo ya Alrosa.
Fedha hizo zilizuiliwa mwanzoni mwa mwaka huu kufuatia vikwazo vya Marekani dhidi ya kampuni hiyo vilivyowekwa Aprili mwaka 2022 na ofisi ya hazina ya Marekani inayodhibiti mali za kigeni.
soma pia:China yaichokoza India kwa ramani mpya rasmi
Baadhi ya wanachama wa kundi la nchi tajiri duniani la G7 wametaka vipitishwe vikwazo vikali dhidi ya biashara ya almasi kwa makampuni ya Urusi.