Iran haitoishambulia Israel iwapo usitishwaji vita utafikiwa
13 Agosti 2024Iran inataka kulipiza kisasi dhidi ya Israel, kufuatia mauaji ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh.
Mmoja wa maafisa hao wa Iran ambaye ni afisa mwandamizi wa usalama amesema Iran pamoja na washirika wake kama Hezbollah watashambulia iwapo mazungumzo ya Gaza hayatopata mwafaka au iwapo Israel itakuwa inajikokota katika suala la upatikanaji wa suluhu.
Shambulizi la Israel laua watu 10 wa familia moja Gaza
Haya yanafanyika wakati ambapo Cyprus imekamilisha maandalizi ya kuwaondoa raia wake nchini Lebanon na Israel.
Haya yamethibitishwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Cyprus, Constantinos Kombos. Mpango unakuja wakati ambapo kuna hofu ya Iran na washirika wake kufanya mashambulizi makubwa hivi karibuni na kuvitanua vita hivyo vya Mashariki ya Kati.