Iran yaanzisha msako wa wanawake wasiofunika vichwa vyao
16 Julai 2023Taarifa ya shirika la habari la Iran IRNA, imemnukuu msemaji wa jeshi la polisi Saeed Montazer Almehdi akisema kuwa polisi wataanzisha msako huo kwa magari na kwa miguu ili kutoa tahadhari, kuchukua hatua za kisheria na kuwapeleka mahakamani wale wote wasiotii amri za polisi na kupuuzia matokeo ya kutokufuata kanuni za mavazi.
Soma pia: Iran yawataka wageni kuheshimu sheria
Iran imechukua hatua hiyo i ikiwa ni miezi kumi tangu kilipotokea kifo cha Mahsa Amini, 22, aliyefariki dunia mikononi mwa polisi kwa kosa kukiuka pia kanuni za mavazi.
Chama cha kihafidhina chenye idadi kubwa ya wabunge na nafasi kubwa katika uongozi kimekuwa kikitetea kanuni za mavazi lakini Wairani wengi wanataka mabadiliko. Mwezi Mei, mahakama na seriikali zilipendekeza muswada wa "kuunga mkono utamaduni wa hijab na usafi" uliochochea mjadala mzito ndani ya taifa hilo.