Israel inaendeleza vita vyake dhidi ya wanamgambo Gaza
24 Desemba 2024Lakini jeshi la Israel linasema limemuua gaidi mmoja hii leo. Kulingana na wizara ya afya ya Palestina mwanamke mmoja wa miaka 53 Khawla Ali Abdullah Abdo aliuwawa katika shambulio la angani katika kambi ya Tulkarem huku kijana wa miaka 18 Fathi Said Awda Ubaid akiuwawa kwa kupigwa risasi kifuani na tumboni. Miili yao imepelekwa katika hospitali ya Thabet.Serikali ya Israel imeshutumiwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika eneo hilo, kuwalenga raia na inayowatambua kama wanamgambo. haijawa wazi ni nani aliyekuwa mwanamgambo kati ya wapalestina hao wawili waliouwawa. Awali Israel kupitia waziri wake wa ulinzi Israel Katz ilikiri kwa mara ya kwanza kuhusika na mauaji ya kiongozi wa kundi la wanamgambo la Hamas Ismail Haniyeh yaliyotokea katika mji mkuu wa Iran, Tehran. Alithibitisha hilo katika taarifa yake kuhusu hatua zaidi wanazochukua dhidi ya kundi la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen, linaloishambulia Israel kwa makombora na droni.Israel ilimuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar Oktoba 16 katika Ukanda wa Gaza, baada ya kuteuliwa na kundi hilo kuchukua nafasi ya Haniyeh aliyeuwawa mjini Tehran. Na mnamo Septemba 27 ikamuua kiongozi wa kundi la wanamgambo la Hezbollah Hassan Nasrallah mjini Beirut nchini Lebanon. Hamas, Hezbollah na Houthis wote wanaungwa mkono na Iran.