1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaanza kujitetea madai ya mauaji ya kimbari ICJ

12 Januari 2024

Israel leo imeanza kujibu shutuma zilizowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ICJ, kwamba operesheni zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza, ni kampeni ya mauaji ya kimbari.

https://p.dw.com/p/4bA42
Uholanzi | Mahakama ya ICJ kuhusu mzozo wa mashairki ya Kati
Mshauri wa kisheria wa wizara ya mambo ya nje ya Israel Tal Becker akiwa ICJPicha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Israel leo imeanza kujibu shutuma zilizowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ICJ, kwamba operesheni zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza, ni kampeni ya mauaji ya kimbari inayoongozwa na serikali ambayo inalenga kuwaangamiza kabisa Wapalestina.

Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa inasikiliza hoja hizo katika siku ya pili, baada ya jana Afrika Kusini kuwasilisha madai yake. Mwanasheria Mkuu wa Israel katika mahakama ya ICJ, Tal Becker, amesema kuwa kesi ya mauaji ya kimbari dhidi yake imepotoshwa sana na haikuakisi hali halisi ya mazingira wakati wa vita vya Gaza.

Soma pia: Afrika Kusini yaishutumu Israel kwa mauaji ya kimbari

Afrika Kusini inaitaka Israel kusitisha mara moja operesheni yake ya kijeshi Gaza. Mahakama ya ICJ iliyoko The Hague, Uholanzi inatarajiwa kutoa uamuzi wake baadae mwezi huu.