Israel yakiri kuhusika na mauaji ya kiongozi wa Hamas
24 Desemba 2024Waziri wa ulinzi wa Israel Israel Katz, amethibitisha hilo katika taarifa yake kuhusu hatua zaidi wanazochukua dhidi ya kundi la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen, linaloishambulia Israel kwa makombora na droni. Katz alisema watashambulia miundo mbinu ya kundi hilo na kuwaua viongozi wao.
"Na tutalishambulia kwa nguvu zote kundi la kigaidi la Houthi linaloishambulia Israel. Tutalenga maeneo yao ya kimkakati, na kuwaua viongozi wao kama tulivyofanya kwa Haniyeh, Sinwar na Nasrallah mjini Tehran, Ukanda wa Gaza na Lebanon, na tutafanya hivyo Hodeida na Sanaa.
Israel ilimuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar Oktoba 16 katika Ukanda wa Gaza, baada ya kuteuliwa na kundi hilo kuchukua nafasi ya Haniyeh aliyeuwawa mjini Tehran. Na mnamo Septemba 27 ikamuua kiongozi wa kundi la wanamgambo la Hezbollah Hassan Nasrallah mjini Beirut nchini Lebanon. Hamas, Hezbollah na Houthis wote wanaungwa mkono na Iran.