1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yamshikilia raia wake mtuhumiwa wa mauaji

19 Septemba 2024

Vyombo vya usalama za Israel vimesema hii leo kuwa vinamshikilia raia wake mmoja anayetuhumiwa kuhusika katika njama ya mauaji yanayowalenga watu mashuhuri nchini humo.

https://p.dw.com/p/4kpHZ
Waziri wa Ulinzi wa Israel Joav Galant
Waziri wa Ulinzi wa Israel Joav GalantPicha: DREW ANGERER/AFP/Getty Images

Mamlaka ya Israel imesema mtu huyo ni mfanyabiashara aliye na uhusiano pia na Uturuki alikamatwa mwezi uliopita, anashukiwa kutumwa na Iran na kwamba alihudhuria angalau mikutano miwili nchini Iran kujadili uwezekano wa kumuua Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant na pia mkuu wa idara ya ujasusi wa ndani. Hii inadhihirisha hali ya kuongezeka mvutano wa mashariki ya kati hasa kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon. Kundi hilo limesema hii leo kuwa wanachama wake 20 wamekufa na wengine 450 wamejeruhiwa kwenye wimbi la pili la milipuko ya vifaa vya mawasiliano.