Israel yashutumiwa kwa mauaji ya halaiki Gaza
10 Agosti 2024Francesca Albanese, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu katika maeneo ya Palestina amesema Israel inawaua Wapalestina kutoka kitongoji kimoja hadi kingine, kwenye hospitali, shule, kambi za wakimbizi na hata kwenye maeneo yanayotajwa kuwa "salama".
Katika mtandao wake wa X, Albanese amesema Israel imekuwa ikifanya mashambulizi hayo dhidi ya Wapalestina kwa kutumia silaha ilizopewa na Marekani na Ulaya.
Hamas: Shambulizi la Israel kwenye shule liliua watu zaidi ya 100
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell pia amesikitishwa na shambulizi hilo lililofanyika katika shule inayowahifadhi wakimbizi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 90 huku wizara ya mambo ya nje ya Misri ikisema mauaji ya raia wa Gaza yanaonyesha kuwa Israel haikuwa na nia ya kusitisha vita.
Misri, Marekani na Qatar wamepanga duru mpya ya mazungumzo ya kusitisha mapigano siku Alhamisi, wakati hofu ikiongezeka ya kutokea mzozo mkubwa zaidi wa kikanda, utakaozihusisha Iran na Lebanon.