1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yatakiwa kupunguza mashambulizi yake Gaza

9 Januari 2024

Israel inakabiliwa na shinikizo linaloongezeka kutoka kwa mshirika wake mkuu Marekani pamoja na mataifa yenye nguvu ya Mashariki ya Kati, ili kupunguza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4b0K9
Eneo la Deir Al-Balah katika Ukanda wa Gaza
Eneo lililoshambuliwa na makombora ya Israel la Deir Al-Balah katika Ukanda wa Gaza: 04.01.2024Picha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Maafisa wa Israel wamesema wanaingia katika awamu mpya ya vita itakayojikita kuwalenga zaidi wapiganaji wa kundi la Hamas, baada ya mashambulizi makubwa ya mabomu ambayo kwa mujibu wa wizara ya Afya huko Gaza, yamesababisha vifo vya Wapalestina zaidi ya 23,000.

Kufuatia mazungumzo na viongozi wa nchi za Kiarabu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema mataifa ya Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Uturuki na yale ya Umoja wa Falme za Kiarabu yameafiki kuanza mipango ya ujenzi na kuandaa utawala wa Gaza mara tu baada ya vita hivyo kumalizika.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema amekuwa akishirikiana na serikali ya Israel na kuihimiza kupunguza mashambulizi yake na kuondoka kabisa katika  Ukanda wa Gaza.