1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yathibitisha kumuua aliyetazamiwa kumrithi Nasrallah

23 Oktoba 2024

Israel imethibitisha Jumatano kuwa ilimuua Hashem Safieddine, aliyetazamiwa kuwa mrithi wa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.

https://p.dw.com/p/4m74P
Lebanon I Hashem Safieddine
Hashem Safieddine, aliyetazamiwa kuwa mrithi wa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.Picha: Bilal Hussein/AP Photo/picture alliance

Taarifa hiyo imesema Safieddine aliuawa wiki tatu zilizopita kufuatia shambulio katika vitongoji vya kusini mwa mji wa Beirut.

Mkuu wa jeshi la Israel Luteni Jenerali Herzi Halevi amesema kama walivyowafikia viongozi waandamizi wa Hezbollah, basi watamfikia yeyote ambaye anatishia usalama wa raia wa Israel. Hata hivyo kundi la Hezbollah halijathibitisha taarifa hiyo.

Hayo yanajiri wakati Israel imeendeleza mashambulizi yake huko Lebanon na katika Ukanda wa Gaza. Umoja wa Mataifa umelaani mauaji ya watu 18 kufuatia mashambulizi ya Israel karibu na Hospitali ya Rafik Hariri mjini Beirut. Jumuiya ya kimataifa imeendelea pia kutoa miito ya usitishwaji mapigano  katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.