1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia kuwa mwenyeji mkutano wa kupunguza wimbi la wahamiaji

22 Julai 2023

Mataifa ya Mashariki ya Kati na yale ya kanda ya bahari ya Mediterania yatakutana kwenye mji mkuu wa Italia, Roma siku ya Jumapili kwa lengo la kuimarisha juhudi za kukabiliana na wimbi la uhamiaji haramu.

https://p.dw.com/p/4UFn0
Wahamiaji wakiwa katika bandari ya Catania, Italia
Wahamiaji wakiwa katika bandari ya Catania, ItaliaPicha: ORIETTA SCARDINO/ANSA/picture alliance

Mwenyeji wa mkutano Italia, imesema washiriki watapendekeza njia za kutanua ushirikiano kwenye sekta za kilimo, miundombinu na Afya kama sehemu ya mkakati wa kukabiliana na uhamiaji.

Taifa hilo limesema mkutano huo utaweka mkakati wa kuyasaidia mataifa ya Afrika ili kupunguza masaibu yanayowalazimisha raia wake kufanya safari hatari kujaribu kuingia Ulaya.

Soma zaidi: Italia yatangaza hali ya dharura kupambana na uhamiaji

Mbali ya Italia, nchi nyingine zitakazoshiriki mkutano huo ni pamoja na Tunisia, Uturuki, Libya, Algeria, Umoja wa Falme za Kiarabu na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na wale wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF. Hata hivyo Ufaransa ambayo ndiyo dola kubwa kwenye kanda ya Mediterrania haitahudhuria mkutano huo.