1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Harris ana uwezo wa kumshinda Donald Trump?

Josephat Charo
23 Julai 2024

Kampeni ya urais ya Kamala Harris imeanza, baada ya rais wa Marekani Joe Biden kujiondoa katika kinyng'anyiro cha kuwania urais na kumuunga mkono Harris awe mgombea wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa Novemba.

https://p.dw.com/p/4idao
President-Elect Joe Biden And Vice President-Elect Kamala Harris Address The Nation After Election Win
Picha: Tasos Katopodis/Getty Images

Kamala Harris amesema atafanya kila analoliweza kukiunganisha chama cha Democratic na kuliunganisha pia taifa la Marekani ili kumshinda Donald Trump. Kukiunganisha chama ni hatua muhimu kwa sababu Harris anasubiri uteuzi rasmi. Harris ndiye mgombea pekee ambaye ataruhusiwa kisheria kutumia mamilioni ya dola za Marekani zilizochangwa na timu ya kampeni ya Biden, kwa kuwa alikuwa sehemu ya tiketi ambayo michango hiyo ilitolewa. Kando na hayo, makamu huyo wa rais anafahamika zaidi kote nchini kuliko wanasiasa wengine wa chama cha Democratic waliotajwa kama watu wambo wangeweza pia kuteuliwa kugombea urais dhidi ya Trump.

Mgombea wa chama cha Democratic Kamala Harris ameingia kwenye kampeni

Lakini kuna mambo ambayo yanamchafulia sifa. Stormy-Annika Mildner, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayotoa ushauri na maoni ya Aspen ya hapa Ujerumani, yenye makao yake makuu mjini Berlin ameiambia DW kwamba udhaifu mkubwa wa Harris ni kwamba umaaarufu wake sio kama ule wa Biden. Jambo lengine ni kuwa, alipewa jukumu la kushughulikia mgogoro wa mpaka na kudhibiti wimbi kubwa la uhamiaji kutoka Amerika ya Kati na Amerika Kusini na amekosolewa na wapinzani kwa kutoifanya kazi hiyo barabara. Hili ni jambo ambalo watu wanaweza kusema alishindwa, jambo ambalo kidogo haitakuwa haki, kwa sababu hali ni ngumu katika eneo la mpaka. Lakini hili ni jambo ambalo kampeni ya Trump italitumia kwa nguvu dhidi ya Harris kwa lengo la kumchafua.

Je, Harris anaweza kumshinda Trump?

Donald Trump na Kamala Harris
Wagombea wa urais wa Marekani, Donald Trump wa chama cha Republican na Kamala Harris wa DemocratsPicha: Evan Vucci/AP/dpa/picture alliance | Shawn Thew/Pool EPA/AP/picture alliance

Donald Trump, mgombea wa chama cha Republican, analazimika sasa kuitoa dira yake kutoka kwa kampeni iliyojikita zaidi juu ya Biden na upinzani dhidi ya rais huyo, ailekeze sasa kwa mgombea mpya aliyeteuliwa kumenyana naye kuwania urais.

Cathryn Clüver Ashbrook, mtaalamu wa mahusiano kati ya Marekani na Ulaya wa wakfu wa Bertelsmann nchini Ujerumani, anasema kwa yale yanayodhihirika katika matokeo ya kura za maoni za awali Harris anakabana koo na Trump au kumshinda kwa asilimia mbili au tatu. Hakuna mengi ya kuzingatiwa kwa sasa, lakini uchunguzi huo wa maoni unaonesha matokeo yasiyobadilibadilika kwamba Harris anawena kumshinda Donald Trump. Na ana uwezo wa kufanya mengi zaidi katika siku zilizosalia kuelekea uchaguzi.

Kamala Harris aungwa mkono kugombea urais Marekani

Wanachama wa chama cha Democtratic wanatumai mgombea mpya atafanikiwa kuleta ari mpya katika kampeni. Mawakili wake wanafikiri anaweza kushinda, kwa kuwa anaweza kuwahamasisha watu ambao hawangejitokeza kwenda kupiga kura kama ingekuwa Biden anagombea, hasa vijana, wanawake na watu wenye asili ya nchi nyingine, nje ya Marekani.

Kigezo kimoja kianchoweza kumsaidia Harris ni wapiga kura wanawake. Tangu mahakama ya juu inayodhibitiwa na idadi kubwa ya mahafidhina kufuta haki ya kikatiba ya kutoa na kuavya mimba, Harris amekuwa akizungumza mara kwa mara kukosoa hukumu hiyo.

Cathryn Clüver Ashbrook, mtaalamu wa mahusiano kati ya Marekani na Ulaya wa wakfu wa Bertelsmann nchini Ujeruman, amesema sauti ya Harris ndiyo iliyokuwa msitari wa mbele kuilinda haki ya mwanamke kuamua. Na amekuwa akipaza sauti kubwa na amefanikiwa katika suala hilo katika kampeni.

Harris anasimama wapi kuhusu NATO, Ukraine na Israel?

Kamala Harris na  Volodymyr Zelensky
Kamala Harris akiwa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Picha: TOBIAS SCHWARZ/AFP/Getty Images

Clüver Ashbrook alisema katika nyanja ya sera za kigeni, Harris bado hajawa na uzoefu mkubwa. Hata hivyo  makamu huyo wa rais aliweka wazi katika mkutano wa usalama wa mjini Munich mwaka huu na mwaka uliopita, kwamba anathamini kwa kiwango kikubwa uanachama wa Marekani katika jumuiya ya kujihami NATO, jambo ambalo Trump ana msimamo tofauti.

Na Harris hataki tu kuendelea kushirikiana na washirika wa Ulaya, bali pia anaona thamani ya miungano ya Marekani katika eneo la Indo-Pasifiki. Na bila shaka ukweli kwamba ana asili ya Kihindi, utakaribishwa katika maeneo kadhaa ya muungano wa Indo-Pasifiki.

Wanasiasa wa Democratic wajitokeza hadharani kumuhakikishia ushindi Harris

Kwa kuzingatia vita vya Ukraine vinavyoendelea, Stormy-Annika Mildner, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayotoa ushauri ya  Aspen ya hapa Ujerumani, yenye makao yake makuu mjini Berlin ameiambia DW kwamba Harris anaamini, kama Biden, kwamba Ukraine inahitaji msaada. Bila shaka kama rais atalazimika kufany akazi pamoja na bunge la Marekani kupata msaada wa fedha na kijeshi, lakini anatarajiw akufanya bidii na kushinikiza midaada hii ipitishe kama alivyofanya Biden, kwa kuwa anaiona Urusi kama kiisho kikubwa.

Mswali kuhusu utakavyokuwa msimamo wa Marekani kuhusu mgogoro wa mashariki ya kati chini ya utawala wa rais Harris, ni muhimu kwa sababu msimamo imara wa Biden kuisadia Israel limekuwa suala la ukosoaji miongoni mwa wapiga kura vijana na hususan Wamarekani wenye asili ya kiarabu.

Mildner anafikiri Harris amekuwa na hujruma zaidi kwa Wapalestina na ametoa kauli nzito kukosoa janga la kibinadamu katika maeneo ya Palestina. Kwa hiyo kauli zinaweza kubadilika kidogo, lakini suala la kusimama pamoja kuinung amkono Israel halitobadilika.

/dw/a-69736650