1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Jeshi la Mali ladhbiti hali Bamako kufuatia shambulizi

Josephat Charo
17 Septemba 2024

Jeshi la Mali limesema linadhibiti hali katika mji mkuu Bamako baada ya kile wanachokiita kuwa ni jaribio la magaidi kutaka kuingia ndani ya kambi ya mafunzo ya jeshi.

https://p.dw.com/p/4kiJf
Mali | Kanali  Assimi Goita
Mtawala wa kijeshi Mali Kanali Assimi GoïtaPicha: OUSMANE MAKAVELI/AFP/Getty Images

Jeshi la Mali limesema katika mtandao wa kijamii kwamba mapema leo asubuhi kundi la magaidi walijaribu kujipenyeza katika kambi ya mafunzo ya jeshi ya Faladie lakini sasa hali imedhibitiwa. 

Baadhi ya maafisa wa usalama ambao hawakutaka kutajwa majina yao walisema milio hiyo ya risasi ilianzia kusikika katika vitongoji kadhaa, ikiwa ni pamoja na maeneo ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa Modibo Keita.

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi kwenye mataifa yote matatu katika miaka ya hivi karibuni watawala wa kijeshi wamevifukuza vikosi vya Ufaransa na kuimarisha mahusiano zaidi na Urusi wakipata masaada wa kijeshi kwa kila nyanja kupitia kundi la mamluki la Wagner. Mashambulizi katikati na kaskazini mwa Mali yameshuhudiwa yakiongezeka.

Soma pia:Zaidi ya watu 10 wameuawa katika shambulio Burkina Faso

Mnamo mwezi Julai takriban wapiganaji 50 wa Wagner waliuwawa katika msafara ulioshambuliwa kwa kushtukiza na wanajihadi wenye mafungamano na al- Qaida na kusababisha hasara kubwa.