1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Jeshi la Marekani lawaua wapiganaji wawili wa IS, Syria

24 Desemba 2024

Jeshi la Marekani limesema limewauwa wapiganaji wawili wa kundi la kigaidi la dola la kiislamu IS nchini Syria na kuwajeruhi wengine

https://p.dw.com/p/4oXr7
Syrien, Manbidsch | Kämpfer der SNA
Picha: Huseyin Nasir/Anadolu/picture alliance

Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani, CENTCOM, imesema wapiganaji hao walikuwa wanasafirisha silaha zilizoharibiwa wakati waliposhambuliwa.

Kamandi hiyo pia imethibitisha tukio hilo kutokea katika eneo lililokuwa awali linadhibitiwa na Utawala wa Syria na Urusi katika mkoa wa Deir al-Zour. Kudhibitiwa huko kulikamilika baada ya utawala wa Bashar al Assad kuangushwa mapema mwezi huu.

Licha ya kundi hilo kuangamizwa mwaka 2019 bado kuna baadhi ya mizizi yake ambayo bado ipo nchini Syria. Marekani inaoongoza muunga wa kimataifa nchini Iraq na Syria katika vita dhidi ya kundi hilo. Na wanajeshi wa muungano huo wanatarajiwa kuebdelea kuwepo nchini Syria hata baada ya Assad kuondolewa madarakani.