Umoja wa Mataifa kupiga kura kupeleka wanajeshi Haiti
2 Oktoba 2023Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuidhinisha wanajeshi hao kutumia nguvu kupambana na magenge yanayosababisha machafuko katika mji wa Port-au-Prince.
Azimio lililoandaliwa na Marekani na kuonekana na shirika la habari la Reuters limetanua vikwazo vilivyowekwa na taifa hilo vinavyotumika tu kwa watu binafsi, kwamba sasa vitawajumuisha pia magenge yote nchini Haiti, jambo ambalo China ilikuwa inaliunga mkono.
Kulingana na maafisa wa Haiti, silaha zinazotumiwa na magenge nchini humo zinaaminika kutolewa Marekani.
Mwaka mmoja uliopita Haiti iliomba msaada wa Kimataifa wa kupambana na magenge hayo. Hata hivyo haijawa wazi iwapo China na Urusi zilizo na kuru ya turufu pamoja na Marekani, Ufaransa na Uingereza watakavyolipigia kura azimio hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu Haiti.