Jeshi la Somalia lawaua wapiganaji 20 Al Shabaab
10 Novemba 2022Duru kutoka Somalia zimearifu kuwa jeshi la nchi hiyo kwa ushirikiano na wanamgambo wa kiukoo wanaoegemea upande wa serikali limewaua wapiganaji wapatao 20 wa kundi la al-Shabaab katika miji ya katikati mwa nchi, katika mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya kundi hilo.
Watu watano wauawa katika shambulio Somalia
Ahmed Shire Falagle, Waziri wa habari wa Jimbo la Galmudug, amesema kufuatia operesheni hiyo, jeshi lilichukua udhibiti wa miji ya El Gorof na Wabho, ambayo ilikuwa ikidhibitiwa na al Shabaab kwa takriban miaka 10.
Watu 100 wauawa kwa mashambulizi ya mabomu Somalia
Al Shabaab yenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al Qaeda imekuwa chini ya shinikizo tangu mwezi Agosti, wakati Rais Hassan Sheikh Mohamud alipoanzisha mashambulizi dhidi yao.
Kundi hilo limewaua maelfu ya watu tangu mwaka 2006, likiwa na dhamira ya kuipindua serikali kuu ya Somalia na kuweka utawala wa sheria kali ya Kiislamu.