1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ukraine lawarejesha nyuma wanajeshi wa Urusi

1 Machi 2024

Jeshi la Ukraine limewarudisha nyuma wanajeshi wa Urusi kutoka kwenye kijiji cha Orlivka kilicho magharibi mwa mji wa Avdiivka, ingawa hali katika eneo hilo bado ni ngumu.

https://p.dw.com/p/4d3qI
Mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine
Hali ilivyo kwenye mji wa Avdiivka ulioko kaskazini mashariki mwa Ukraine, ambao unawaniwa kati wa wanajeshi wa Urusi na Ukraine.Picha: TASS/dpa/picture alliance

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram, mkuu wa jeshi la Ukraine, Oleksandr Syrskyi, alisema majeshi ya Urusi bado yanaendelea na mashambulizi katika maeneo mengi na kwamba hali ni tete hasa katika maeneo ya Avdiivka na Zaporizhzhia.

Soma zaidi: Urusi yaandaa mashambulizi mapya dhidi ya Ukraine

Kijiji cha Orlivka kiko chini ya kilomita mbili kaskazini magharibi mwa Lastochkyne, eneo ambalo wiki hii lilitekwa na majeshi ya Urusi.

Wiki iliyopita, majeshi ya Urusi yaliuteka mji wa mashariki mwa Ukraine wa Avdiivka baada ya mwezi mzima wa mapambano na wanashinikiza kuteka maeneo mengine katika mstari wa mbele wa mapambano.