1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Josep Borrell afanya ziara fupi Kyiv

9 Novemba 2024

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Joseph Borrell, yuko mjini Kyiv kuihakikisha Ukraine kwamba Umoja huo inaiunga mkono.

https://p.dw.com/p/4mpLH
Umoja wa Ulaya | Josep Borrell
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Joseph BorrellPicha: FREDERICK FLORIN/AFP

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja huo tangu Donald Trump kushinda uchaguzi wa Marekani. 

Ushindi wa kiongozi huyo wa chama cha Republican umeleta wasiwasi nchini Ukraine na Ulaya kwa Ujumla kwamba Trump anaweza kusitisha msaada wa Marekani kwa Kyiv katika vita vyake kupinga uvamizi wa Urusi nchini humo. 

Baerbock awasili Kiev kusisitiza mshikamano

Borrell amesema ujumbe uko wazi kabisa kwamba wameiunga mkono Ukraine kuanzia mwanzo na wataendelea kufanya hivyo kwa muda wote. 

Wakati wa kampeni zake, Trump alionesha mashaka ya kuendelea kuiunga mkono kijeshi na kifedha Ukraine akisema anaweza kuwa na makubaliano ya haraka ya kusitisha vita kati ya mataifa hayo mawili.