1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamanda mkubwa wa kijeshi wa Urusi auawa Moscow

17 Desemba 2024

Uchuguzi wa Urusi waonesha pikipiki iliyokuwa karibu na jengo moja mjini Moscow liliripuka na kumuua kamanda wa kitengo cha kemikali na kibaolojia cha wanajeshi wa Urusi, Jenerali Igor Kirillov, pamoja na msaidizi wake.

https://p.dw.com/p/4oEcR
Russland, Moskau | Explosion in Wohnblock auf der Ryazansky Prospekt Straße
Huduma za dharura zinaonekana kwenye eneo la mlipuko kwenye jengo la ghorofa kwenye Mtaa wa Ryazansky Prospekt. Picha: Mikhail Metzel/TASS/IMAGO

Msemaji wa kamati hiyo, Svetlana Petrenko, amesema wanaendelea na uchunguzi kujua namna tukio hilo lilivyopangwa, zaidi amesema "Idara ya usalama wa taifa ya Ukraine, SBU, mnamo Desemba 16, ilimshitumu Kirillov kutumia silaha za sumu zilizopigwa marufuku, wakati wa operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine ilioanza Februari 2022". Mwezi Mei, Marekani pia iliishutumu Urusi kwa kutumia sumu aina ya chloropicrin dhidi ya wanajeshi wa Ukraine kinyume na Mkataba wa Silaha za Kemikali (CWC). Urusi imekanusha tuhuma hizo na kusema haimiliki tena aina hiyo ya silaha za kemikali.