1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Kambi ya Wagner yashambuliwa kwa droni nchini Libya

30 Juni 2023

Kambi ya kijeshi inayotumiwa na mamluki wa Urusi wa Wagner imeshambuliwa na droni mashariki mwa Libya, lakini haikusababisha maafa yoyote. Hadi sasa haijafahamika wazi ni nani aliyehusika na shambulio hilo.

https://p.dw.com/p/4TGu8
Wagner-Gruppe in Libyen
Picha: US Africa Command/AFP

Afisa mmoja wa kijeshi kwa sharti la kutotajwa jina ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mashambulizi hayo yaliendeshwa usiku kucha katika kambi yenye uwanja wa ndege ya Al-Kharruba takriban kilomita 150 kusini magharibi mwa mji wa Benghazi.

Mamluki wa Urusi wa Wagner wanaendesha shughuli zao katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta na ambalo limekumbwa na zaidi ya muongo mmoja wa mzozo tangu kuondolewa madarakani kwa Moamar Kadhafi.

Libya imegawanyika kati ya serikali mbili, mmoja ikiwa ni ya mpito mjini Tripoli na nyengine ya mashariki inayoungwa mkono na Khalifa Haftar. Makundi mengi ya wapiganaji wa kigeni kutoka Chad, Sudan, Niger na Syria bado yanaripotiwa nchini humo.