KAMPALA Bunge lamuunga mkono Museveni
29 Juni 2005Matangazo
Bunge nchini Uganda lilipiga kura kufutilia mbali mpaka wa rais kuweza kuitawala nchi hiyo, hivyo kudhihirisha kumuunga mkono rais wa sasa Yoweri Museveni, kuwania wadhifa wa urais katika uchaguzi ujao. Ijapo uamuzi huo unahitaji kura nyengine kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao, ilikuwa mara ya kwanza kwa wabunge kuulizwa kuupigia kura mpango huo.
Matokeo ya kura hiyo yamewashangaza baadhi ya raia ikiwa ni pamoja na waandamanaji kadhaa waliofanya maandamano nje ya majengo ya bunge, wakipinga hatua ya bunge kumtaka Museveni aendelee kuwa raisi wa taifa hilo.