1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Kampeni za uchaguzi Pakistan kuhitimishwa leo

6 Februari 2024

Wagombea wa viti mbalimbali nchini Pakistan leo wanafanya kampeni kwa mara ya mwisho kuelekea uchaguzi wa Alhamisi wiki hii ambao waangalizi wanasema umeliacha taifa hilo la watu milioni 240 katika hali ya kukata tam

https://p.dw.com/p/4c5dF
Mabango ya kampeni nchini Pakistan
Mabango ya kampeni nchini PakistanPicha: Tanveer Shahzad/DW

 

Wagombea wana hadi leo usiku kuwashawishi wapiga kura kabla ya kufanyika uchaguzi huo siku ya Alhamisi ambapo zaidi ya watu milioni 120 wamesajiliwa kama wapiga kura.

Uchaguzi huo unafanyika wakati waziri mkuu wa zamani akiwa gerezani na chama chake kimezuiwa kugombea, na hivyo kukifungulia njia chama cha Pakistan Muslim League kushinda viti vingi bungeni na kumpa fursa ya kuhudumu kwa muhula wa nne kama Waziri Mkuu mwanzilishi wake Nawaz Sharif. 

Vyama 44 vya kisiasa vitawania viti 266 katika bunge la kitaifa huku kukiwa na viti maalum 70 vya ziada vilivyotengwa kwa ajili ya wanawake na jamii ya walio wachache.