1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz afanya mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping

3 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amefanya mazungumzo kwa njia ya video na Rais wa China Xi Jinping, kujadili masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili pamoja na mzozo wa Mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/4YNuL
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na mwenzake wa China Xi Jingping
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na mwenzake wa China Xi JingpingPicha: Kay Nietfeld /AFP

Scholz na Xi wamejadili pia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kusisitiza kwamba mgogoro huo haupaswi kugeuka na kuwa vita vya nyuklia, huku wakikumbushia kwamba vita vya aina hiyo havina mshindi.

China yasema Beijing inapendelea ushirikiano na Ujerumani

Hapo jana, Rais wa Urusi Vladimir Putin ameiondoa nchi yake katika makubaliano yanayopiga marufuku majaribio ya silaha za nyuklia, na hivyo kutoa uwezekano kwa Moscow kuanzisha mazoezi ya aina hiyo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo kadhaa.