Biashara
Kenya, EU zasaini makubaliano "ya kihistoria" ya biashara
18 Desemba 2023Matangazo
Hayo yamefahamishwa na Rais William Ruto katika wakati ambapo Brussels ikilenga kukuza mahusiano ya kiuchumi na bara la Afrika.
Ruto amesema huo ni mwanzo wa ushirikiano wa kihistoria utakaopelekea pia mabadiliko ya kihistoria. Rais huyo wa Kenya aliyasema hayo katika hafla iliyohudhuriwa na rais wa Hamlashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Soma pia: Kenya inatafuta utulivu wa kiuchumi baada ya miaka 60 ya uhuru
Von der Leyen amesema ushirikiano huo ni wa manufaa kwa pande zote mbili na kutoa wito kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki kujiunga na makubaliano hayo ya ushirikiano wa kiuchumi.